
Mtandao wa Twitter umesema kuwa unafanyia kazi kitufe cha kuhariri (Edit Button), kipengele ambacho kitawaruhusu watumiaji kubadili tweets zao baada ya kuzichapisha.
.
Hatua hiyo inafuata baada ya Mjumbe mpya wa Bodi ya Kampuni hiyo ambaye pia ni Bosi wa Kampuni ya TESLA, Elon Musk, kuwauliza wafuasi wake katika kura ya maoni ya Twitter kama walitaka kitufe hicho.
