Back to top

Uandaaji Bajeti kuzingatia masuala ya kijinsia

22 April 2022
Share

Naibu Katibu Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw.Kaspar Mmuya amesema serikali itaendelea kusimamia uandaaji wa bajeti unaozingatia masuala ya kijinsia kama sehemu ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia  mafunzo ya Uandaaji wa Bajeti zinazozingatia Usawa wa Kijinsia yaliyotolewa  kwa Wakurugenzi na Wakuu  wa Vitengo kutoka (Ofisi ya Waziri Mkuu Sea, Bunge na Uratibu)  yaliyofanyika Aprili 20, 2022  katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Dodoma.


Bw.Mmuya ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Uandaaji wa Bajeti zinazozingatia Usawa wa Kijinsia ili kuwajengea uwezo wakurugenzi na wakuu wa witengo kutoka ofisi hiyo yaliyofanyika Dodoma.