Back to top

Ubovu wa miundombinu ya viwanja wakwamisha vipaji- Kagera.

12 June 2021
Share

Zaidi ya wanafunzi mia tano wa shule za sekondari mkoani Kagera zilizofanikiwa kuingia kambini kwa lengo la kutengeneza timu mbalimbali za kuwakilisha wenzao katika mashindano ya UMISETA ngazi ya taifa huko mkoani Mtwara wameiomba serikali kuwaboreshea miundombinu ya viwanja na vifaa ya michezo mashuleni ili kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao na michezo.

Wakizungumza katika mashindano ya UMISETA ngazi ya mkoa wa kagera, baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za ubovu wa miundombinu ya viwanja, pamoja na  vifaa vya michezo.

Afisa michezo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Keffa Elias amesema serikali kupitia halmashauri nane za mkoa wa Kagera tayari zimekwisha tenga maeneo maalumu ya kutengeneza viwanja vya michezo katika tasisi za umma zikiwemo shule kwa lengo la kuendelea kukuza vipaji huku katibu tawala wa mkoa wa Kagera.