Back to top

Uchafuzi wa hewa, vifo milioni 7 kwa mwaka.

23 September 2021
Share

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeimarisha miongozo yake ya ubora wa hewa huku likisema uchafuzi wa hewa kwa sasa ni moja ya kitisho kikubwa ambacho kinasababisha vifo milioni 7 kwa mwaka na kwamba hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kupunguza uchafuzi huo. 

Miongozo hiyo ina lengo la kusaidia kuwalinda watu na madhara ya uchafuzi wa hewa na inatumiwa na serikali kama kumbukumbu ya makubaliano yanayopaswa kutekelezwa. 

Mara ya mwisho WHO kutoa miongozo kuhusu ubora wa hewa ilikuwa 2005, ambazo zilikuwa na matokeo mazuri katika sera za kupunguza uchafuzi wa hewa ulimwenguni. 

Hata hivyo, WHO imesema katika miaka hiyo 16 ushahidi mkubwa umeonesha jinsi uchafuzi wa hewa unavyoathiri afya, kuliko ilivyoeleweka awali.