Back to top

Uchaguzi wa Rais na wabunge kufanyika leo Burundi.

20 May 2020
Share

Wananchi wa Burundi leo Jumatano wanapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wengine wakiwemo wabunge katika uchaguzi unaofanyika licha ya nchi hiyo kukabiliwa na janga la Corona.

Huu ni uchaguzi ambao unawakutanisha wagombea saba wanaotafuta urais, kuchukua nafasi ya rais Pierre Nkurunziza ambaye hawanii tena baada ya kuwa madarakani kwa miaka 15.

Wachambuzi wa siasa wanasema ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala CNDD-FDD Jenerali Evariste Ndayishimiye, na kiongozi wa zamani wa waasi Agathon Rwasa, kutoka chama kikuu cha Upinzani CNL.

Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema wapiga kura zaidi ya Milioni tano wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu.