Back to top

Uchimbaji wa jadi migodini wachangia ongezeko la maambikizi ya TB

28 November 2019
Share

Uchimbaji wa kutumia njia za jadi  unaofanyika katika migodi mbalimbali ya madini hapa nchini umetajwa kuwa chanzo kikuu cha ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa wachimbaji wadogo.

Akizungumza jijini Arusha mratibu wa kifua kikuu maeneo ya migodini Dkt. Allan Tarimo amesema tafiti zinaonyesha kuwa  kasi ya maambukizi katika maeneo ya migodi ni mara kumi zaidi ya maeneo ya kawaida.

Dkt.Leonard Subi ni mkurugenzi wa kinga wizara ya afya ,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto amesema ongezeko la vituo vya upimaji wa kifua kikuu sugu ambavyo baadhi vipo  jirani na maeneo ya migodi vimesaidia kukabiliana na tatizo