Back to top

Uchumi wa kati 2025 kutofikiwa kutokana na uharibifu wa mazingira.

19 September 2019
Share

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imesema mpango wa taifa wa uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hauwezi kufikiwa endapo vitendo vya uharibifu wa mazingira vitaendelea kushamiri nchini.

Kamati hiyo imeitaka serikali kuzipa meno mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria na sera ya mazingira ili kudhibiti matukio hayo.

Wakizungumza katika kongamano kuelekea kilele cha siku ya Amani Duniani wabunge wajumbe wa kamati hiyo wamesema uharibifu wa mazingira una athari kwa maendeleo kwani unagusa nyanja zote ikiwemo afya, amani na kilimo ambazo ndio nyenzo kuu ya kufikia uchumi huo.

Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, Bibi Clara Makenya amesema ongezeko la magonjwa ya Malaria na Kipindupindu hasa kwenye nchi za ukanda wa tropiki ikiwemo Tanzania ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi.