Back to top

Ufaransa yaipatia Tanzania Bilioni 175.6 .

27 May 2020
Share

Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa shilingi bilioni 175.6  kati yake na Shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa ajili ya miradi ya maji safi na majitaka mjini Morogoro ambapo fedha hizo zimeelekezwa katika mkoa huo.
 
 
Akisaini mkataba huo jijini Dodoma Katibu Mkuu wa wizara ya fedha na mipango Bw Dotto James amesema mpaka sasa Shirika la maendeleo la Ufaransa imeshaifadhili Tanzania katika sekta za maji na nishati miradi ya takribani shilingi bilioni 387.6.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Stephanie Mouen Essombe amesema hatua hiyo ni muendelezo wa ushirikiano wa mataifa haya mawili uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.
 
Awali akizungumza wakati wa zoezi hilo Katibu Mkuu wizara ya maji Prof Kitila Mkumbo amesema utekelezaji wa mradi huo utaenda sambamba na upanuzi wa bwawa la Mindu.