Back to top

Ufaulu duni hausababishwi na ukosefu wa walimu - TAMISEMI

06 November 2019
Share

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Mwita Waitara amesema si kweli kwamba ufaulu duni wa shule za sekondari katika masomo ya sanaa umesababishwa na hatua ya serikali kuhamisha walimu hao kwenda kufundisha shule za msingi mwaka wa fedha 2017/18 ambapo walimu zaidi ya elfu 8 walihamishwa.

Waziri Waitara amesema hayo wakati akijibu swali la Mhe.Salome Wycliffe Makamba (Viti Maalum) aliyetaka kujua juu ya sababu za kitaalam zinazosababisha walimu wa shule za sekondari kuhamishiwa shule za msingi wakati ufaulu wa masomo ya sanaa kwa shule za sekondari ukiwa duni. 

Amesema ufaulu duni husababishwa na masuala mbalimbali kama mazingira, uelewa wa wanafunzi, ushiri wa wazazi na jamii katika mchakato mzima wa ufunzaji na si walimu pekee na kwamba.
 
Serikali ilifanya uhamisho huo wa walimu wa masomo ya sanaa kutokana na ziada ya walimu hao katika shule za sekondari wakati shule za msingi zikiwa na uhaba na hakuna shaka juu ya uwezo wa walimu katika kufundisha kwani kitaalamu walimu ngazi zote huandaliwa kwa mfanano katika mbinu za  kufundisha.  

Hata hivyo amesema wizara imeomba kibali cha kuajiri walimu wapya elfu 22 ili kupunguza uhaba wa walimu uliopo katika shule za msingi na sekondari.