Back to top

Uganda yafunga hospitali 1 baada ya watu 19 kuambukizwa Corona

25 September 2020
Share

Serikali ya Uganda imeifunga hospitali moja ya wilaya Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya wafanyakazi kumi na tisa kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Kitengo cha wajawazito cha kujifungulia pamoja na maabara havijafungwa ili kutoa huduma za dharura.

Wizara ya Afya imesema imechukua hatua hiyo ili kudhibiti maambukizi zaidi wakati huu nchi hiyo ikiwa na maambukizi zaidi ya elfu sita na mia saba.

Waziri wa Afya Jane Ruth Acieng amesema kuelekea kufunguliwa kwa shule mwezi ujao, jitihada zinafanyika kuwapima walimu virusi vya Corona.

Wakati huo huo, Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa John Mkengasong amezipongeza nchi za Afrika kwa kuweza kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona.