Back to top

Ugiriki yaendelea kukabiliwa na joto kali.

01 August 2021
Share


Ugiriki inaendelea kukabiliwa na wimbi la joto kali wakati wazima moto wakiendelea kupambana na moto uliosababishwa na ukame katika maeneo mbalimbali.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha serikali, watu 16 wametibiwa katika hospitali kwenye rasi ya Peloponnese, Kusini mwa Ugiriki kutokana na matatizo ya kupumua.

Nyumba kadhaa katika eneo la mji mdogo wa Egion ziliharibiwa  na kufikia leo asubuhi moto huo ulikuwa umedhibitiwa.

Hata hivyo kikosi cha ulinzi wa raia kimeonya kuwa hatari ya moto inabaki juu kutokana na ukame.

Wakati hayo yakiarifiwa matetemeko mfululizo ya ardhi yametikisa Visiwa vya Dodecanese Kusini-Mashariki mwa Bahari ya Aegean nchini Ugiriki.