Back to top

Ugonjwa wa michubuko waathiri mifugo Geita.

13 December 2019
Share

Wafugaji mkoani Geita wameiomba Wizara ya mifugo na uvuvi iwasaidie kudhibiti ugonjwa hatari  wa michubuko kwa mifugo yao ulioibuka hivi karibuni na kuathiri idadi kubwa mifugo ambayo inasababisha ngozi ya ng’ombe kuwa na vidonda sehemu zote za mwili  hali inayowatia hofu ya kupoteza mifugo yao.


ITV imefika eneo la Lukaya   kata ya Kiyambo na kushuhudia maelfu ya mifugo ikiogeshwa katika majosho mbalimbali huku idadi kubwa ya mifugo ikionekana kuathirika na ugonjwa huo kisha wafugaji wakaeleza namna ambavyo mifugo yao imeathirika.

Akiongozana na wataalamu wa kudhibiti magonjwa ya mifugo kufika eneo hilo daktari wa mifugo kanda ya ziwa dokta Rosamystica Sambu amewataka wafugaji kuondokana dhana potofu juu ya magonjwa ya mifugo badala yake waogeshe mifugo yao ili kukinga mifugo na magonjwa. 

Akizungumza na wafugaji katika zoezi hilo la uogeshaji mifugo mratibu wa  uogeshaji mifugo kutoka wizara ya mifugo na uvuvi dokta Aurelia Bundala amesema ugonjwa huo ni hatari kwa mifugo na serikali imeanza kuchukua hatua ili kuudhibiti ugonjwa huo.