Back to top

Ugonjwa wa mnyauko wawatia hofu wakulima

14 April 2019
Share

Wakulima wa mazao ya mbogamboga katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa kaskazini wameingiwa na hofu ya kupata mavuno yasiyokidhi gharama wanazotumia  kutokana na kuonekana kwa ugonjwa wa mnyauko unaoathiri zao la Nyanya.

Wakulima katika kijiji cha Kikwe kilichopo wilayani Arumeru ni miongoni  mwa walioathiriwa na ugonjwa huo wakieleza kuwa  wanalazimika kujaribu  dawa za aina mbalimbali kukabiliana nao  ambazo hata hivyo  wataalamu wa kilimo  wanawashauri kutokuzitumia  bila kupata maelekezo ya kitaalamu.

Ugonjwa huo wa mnyauko unakuja wakati bado ugonjwa wa nyanya  unaojulikana kama Kanitangaze ukiwa haujapatiwa suluhisho la kudumu,huku wakulima hao pia wakieleza kukabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji hususani wakati wa msimu wa kiangazi

Akizungumzia changamoto  ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji wakati wa maonyesho ya siku ya mkulima iliyofanyika    katika moja ya shamba darasa la kilimo cha nyanya lililopo kijijini  kikwe,mkurugenzi mtendaji wa asasi kilele inayoendeleza kilimo  cha horticulture hapa nchini –TAHA Jackiline Mkindi anasema jitihada zinafanyika kwa kushirikiana na wadau kuwajengea uwezo wakulima kutumia teknolojia ya umwagiliaji kwa njia ya matone