Back to top

Uhaba wa vyoo kwenye ukumbi wapelekea Madiwani wajisaidia vichakani.

09 May 2021
Share

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga hasa wenye ulemavu wapo hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupindu  kutokana na ukumbi wanao utumia kwa ajili ya mikutano kuwa na uhaba wa matundu ya vyoo hali inayopelekea kujisaidia  kwenye vichaka vilivyopo karibu na ukumbi huo.

Pamoja na kukiri uwepo wa changamoto hizo kwenye ukumbi huo Mkuu wa Wilaya Bi.Kissa Kasongwa amesema hilo lipo nje ya uwezo wake na hivyo atafikisha kilio hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw.Martine Shighela ili alitolee ufafanuzi.