Back to top

Uhamiaji kuwafundisha elimu ya uraia wanafunzi wenye Ualibino

23 March 2018
Share

Ofisi ya Idara ya Uhamiaji Mkoani Shinyanga imeanza mpango maalum wa kuwafundisha elimu ya uraia, wanafunzi wenye Ualibino wanaosoma katika Shule ya Msingi Buhangija Mchanganyiko lengo likiwa ni kuwafanya wakue wakiwa wanajitambua kuwa ni raia wa taifa la Tanzania.

Afisa Uhamiaji Mkoani Shinyanga, Bwana BASHIRI MANG'ENYA amesema lengo la kutoa elimu ya uraia kwa watot hao ni kuhakikisha kundi hilo linajitambua haki na wajibu wao wa kiraia.

Baadhi ya watoto wenye ualibino katika Kituo cha Walemavu Mchanganyiko cha Buhangija wamesema elimu hiyo inayoendelea kutolewa na Maofisa wa Uhamiaji itawasaidia na wa meahidi kuendelea kujifunza somo la Uraia.

Bibi. MWINJI NYONDWA ni afisa uhamiaji mwanamke amewataka watoto wakike wanaoishi katika kituo hicho cha Buhangija kufanya bidii katika masomo yao ili wapatikane wataalamu wengi zaidi wa kike.