
Serikali imeahidi kujenga usiku na mchana daraja la Mkange lililopo eneo la Kiegeya wilayani Kilosa katika barabara kuu ya Morogoro Dodoma ili kuhakikisha mawasiliano yaliyokatika yanarejea kama kawaida ndani ya muda mfupi ujao.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare aliyefika eneo la tukio na kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa na kuungana na ile ya Gairo iliyokuwa upande mmoja wa barabara na ya Kilosa upade wa pili wa daraja amesema tayari wamefanya mawasiliano wizara ya ulinzi na wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasilaino ambao wamechukua hatua kuwaongezea nguvu ya wataalamu na vifaaa kufanikisha ksazi hiyo kwa wakati.
