Back to top

UJUMBE WA TANZANIA KAMATI YA SIASA NA DIPLOMASIA YA SADC

09 February 2024
Share

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.Samwel Shelukindo, ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kamati ya Siasa na Diplomasia (Inter-State Politics and Diplomacy Committee — ISPDC) ya SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Zambia, Bi.Etambuyu Gundersen, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.

Mkutano huo uliitishwa kujadili masuala ya kisiasa na Diplomasia katika kanda, aidha Mkutano umetoa salamu za pole kwa Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Namibia kufuatia kifo cha Hayati Dkt. Hage Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichotokea hivi karibuni.