Back to top

UJUMBE WA TANZANIA KIKAO KAMATI YA FEDHA SADC

15 March 2022
Share

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedaha na Mipango Bi.Amina Shaabani ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kikao cha kamati ya fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Ajenda zilizojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kuidhinishwa kwa bajeti ya kutafsiri kwa Kiswahili vitabu vilivyoandikwa na Hashim Mbitta kuhusu harakati za ukombozi kusini mwa Afrika na ujenzi wa sanamu ya kumbukumbu ya Hayati Julius Nyerere ili kuenzi mchango wake katika ukombozi na maendeleo katika ukanda wa nchi za SADC