Back to top

UKALI BEI YA MAFUTA NCHINI RAIS SAMIA AVUNJA UKIMYA

09 May 2022
Share

Rais Samia ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Taifa kuhusu namna ya kukabiliana na suala la kupanda kwa bei ya Mafuta nchini.

Mhe. Rais Samia ameongeza kuwa Serikali imesikia kilio cha wananchi kuhusu ukali wa maisha unaotokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa mbalimbali ambapo amebainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha serikali anayoiongoza itachukua hatua mbalimbali za kikodi kuweka ahueni kwa wananchi" Rais Samia Suluhu Hassan. 

TUJIKUMBUSHE.

Usiku wa Mei 08, 2022 Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan aliitisha Kikao cha dharura Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Ambapo kikao hicho alikuwepo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia alitoa maaagizo kwa viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.