Back to top

UKIPOTOSHA BANGO LA BAKITA JELA MIAKA 3.

23 February 2022
Share

Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limekemea vikali watu wanaotumia nembo ya Baraza hilo kwa kupotosha mabango yenye misamiati yenye maudhui mbalimbali ya Kiswahili kutoka Baraza hilo kwa kuandika maneno yao na kuyasambaza mtandaoni, ambapo atakaye bainika atalipa faini isiyopungua Milioni 5 au kutumikia kifungo kisichopungua miaka 3 ama vyote kwa pamoja. taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BAKITA Bi.Consolata Mushi.