Back to top

Ukosefu wa walimu wa sayansi na maabara mwiba mchungu Kasulu

18 October 2019
Share

Wanafunzi wa shule za sekondari katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma,wamelalamikia shule zao kukosa walimu wa sayansi na vyumba vya maabara kutokamilika na vingine kutumika kwa kazi nyingine ikiwa ni pamoja na kugeuzwa kuwa madarasa hali inayosababisha washindwe kusoma kikamilifu masomo ya sayansi.

Wanafunzi hao wamemweleza waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Mhe.Profesa Joyce Ndalichako kwa nyakati tofauti baada ya kutembelea shule za sekondari Kigodya na Kasangezi.

Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Mhe.Profesa Joyce Ndalichako amesema azma ya serikali ni kuhakikisha shule zote zinakamilika kwa vifaa,walimu na miundombinu na kwamba wizara imekuwa ikitoa fedha za miundombinu hivyo ni jukumu la viongozi wa wilaya na mikoa kusimamia na wanafunzi kusoma kwa bidii