
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema kuwa Raia wa Ukraine kwa sasa ni kundi kubwa la pili la wakimbizi duniani, baada ya Syria yenye wakimbizi zaidi ya milioni 6.8, ambapo mpaka sasa raia milioni tano wa Ukraine wameondoka nchini humo katika kipindi cha chini ya miezi miwili tangu wanajeshi wa Russia walipoanza vita nchini Ukraine ambapo raia hao wengi wametafuta hifadhi katika nchi jirani za Ulaya ambako wanapewa ulinzi wa muda na huduma mbalimbali.
