Back to top

ULEGA AKABIDHI VIFAA VYA SHULE KWA YATIMA

12 February 2024
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, amekabidhi vifaa vya shule kwa Wanafunzi Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wilayani Mkuranga, mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuinua maendeleo ya elimu wilayani humo.

Vifaa alivyokabidhi ni Madaftari, Viatu, Mabegi na Mashine za Photocopy ambavyo vyote vimegharimu Shilingi Milioni 42 na kunufaisha wanafunzi takriban 300.

Pia, Waziri Ulega ametoa motisha kwa wanafunzi waliopata matokeo mazuri katika masomo yao ya kidato cha nne waliokuwa wanasoma katika shule zilizopo wilayani Mkuranga.