Back to top

Ulinzi waimarishwa Kuelekea Royal Tour. 

27 April 2022
Share

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine Masejo amewaambia wananchi kuwa hali ya ulinzi na usalama katika jiji la Arusha na mkoa ni shwari kuelekea uzinduzi wa filamu ya Royal Tour.

Kamanda Masejo amesema kuwa Kuelekea uzinduzi wa filamu maalum ya The Royal Tour Tanzania kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limejianga vyema kuhakikisha dunia inashuhudia uzinguzi huo wa filamu ya  Royal Tour itakayofanyika siku Aprili 28, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionyesha dunia ukarimu huo na kuionyesha dunia kuwa Arusha ni kitovu cha utalii.