Back to top

UMMY: 85% YA VIFO VYA UZAZI, VINA UHUSIANO NA MAPUNGUFU YA UJUZI

05 March 2024
Share

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, amesema ni muhimu kuendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma za Afya kwani taarifa zinaonesha kuwa kati ya vifo 100 vinavyotokana na uzazi, takribani 85% ya vifo hivyo vina uhusiano na mapungufu ya ujuzi “skills incompetence” kwa baadhi ya watoa huduma za afya.
.
Waziri Ummy ameyasema hayo  wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi 110 kutoka katika vituo 25 vinavyotoa huduma ya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (CEMONC), ambapo amesisitiza kuwa kipaumbele chao kwa sasa ni watoto wachanga na kwamba hataki kusikia mambo ya mtoto si riziki kwani yamepitwa na wakati.
.
Waziri Ummy amewataka wakufunzi hao kwenda kuwajengea uwezo wenzao waliobaki katika vituo kwani lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha ujuzi wa watoa huduma za Afya ya mama na mtoto hususani watoto wachanga.
.
Aidha, Mhe.Ummy amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kutoa takwimu sahihi za vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, chini ya mwaka mmoja pamoja na vifo vya watoto wachanga wenye umri wa chini ya siku 28.