Back to top

UMMY: SARATANI HUSABABISHA VIFO 26,000 KILA MWAKA

07 February 2024
Share

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, amewataka Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa saratani kwani kila mwaka wagonjwa wa saratani 40,000 hugundulika na husababisha vifo 26,000.
.
Mhe.Ummy ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa maendeleo, kwa ajili ya uanzishwaji wa kituo cha umahiri cha matibabu ya Saratani nchini kilichofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Jijini Dar Es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa endapo tahadhari haitachukuliwa, vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vitaongezeka.
.
Mhe.Ummy amesema zaidi ya 80% ya wagonjwa wa Saratani wanaofika hospitali hali zao zinakua katika hatua ya Tatu hadi hatua ya Nne hali ambayo husababisha ugumu wa matibabu tofauti na ambavyo angewahi kujua hali yake na kuanza matibabu mapema.
.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Ummy amewataka Watanzania wapime Saratani angalau mara moja kwa mwaka kwa kuwa Saratani inayoongoza ni ya mlango wa kizazi kwa 25%, matiti 10%, tezi dume 9% na mfumo wa chakula 6.5%.