Back to top

UN kupiga kura kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya Eritrea

14 November 2018
Share

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linataraj ia kupiga kura kuondoa vikwazo vya silaha vilivyochukuliwa miaka kumi iliyopita dhidi ya Eritrea baada ya uamuzi wa nchi hiyo kufufua uhusiano na Ethiopia.

Wajumbe kutoka nchi kumi na tano wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walihitimisha mazungumzo yao siku ya Jumatatu na walikubaliana kuhusu rasimu ya azimio iliyotolewa na Uingereza ili kuondoa vikwazo vinvyoisibu Eritrea tangu mwaka 2009.