Back to top

UN yataka kuachiliwa wahandisi wa kigeni waliotekwa nyara mara moja.

23 July 2018
Share

Mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa ametoa wito wa kuachiliwa mara moja bila masharti yoyote wahandisi wa kigeni waliotekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana kwenye kisima cha mafuta kusini mwa Libya.

Naibu mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kisiasa Bibi Stephanie Williams amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na mwenyekiti wa Kampuni ya mafuta ya taifa ya Libya Bw. Mustafa Sanalla huko Tripoli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolwa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya, Bibi Williams amelaani utekaji nyara huo na kutoa wito wa kuachiliwa wafanyakazi hao mara moja bila masharti yoyote.

Katikati ya mwezi Julai, watu wenye silaha wasiojulikana waliwateka nyara wahandisi wanne wakiwemo waLibya watatu na Mromania mmoja wanaofanya kazi katika kisima cha mafuta cha Sharara, kusini mwa Libya.