Back to top

UNICEF yataka msaada wa kimataifa kwa ajili ya elimu ya watoto Syria.

24 April 2018
Share

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeonya kuwa, licha ya fedha nyingi zilizotolewa katika miaka saba iliyopita, mamilioni ya watoto na vijana nchini Syria bado wanakabiliwa na hatari ya kuacha shule.

UNICEF imetaka kuwepo kwa misaada ya kimataifa ya muda mrefu, yenye unyumbufu na isiyo na masharti kwa ajili ya elimu ya watoto na vijana wa Syria.

Kwa mujibu wa UNICEF, asilimia 90 ya watoto wanasoma katika shule za umma, nchini Syria na katika nchi jirani. Watoto wa Syria pia wanaweza kujiunga na shule za umma nchini Lebanon na Jordan.

Mgogoro uliodumu kwa miaka saba umesababisha watoto milioni 2.8 kukosa elimu. Baadhi yao hawapati nafasi ya kujiunga na shule, wengine wamekosa masomo kwa miaka saba na ni ngumu kwao kuwafikia wenzao.