Back to top

UONGOZI THE CASK BAR UMEKIUKA MASHARTI YA LESENI

17 August 2023
Share

Kufuatia sakata la kufungwa kwa Baa ya The Cask Bar & Grill kwa muda wa siku 30, iliyopo katika eneo la kibiashara la Rock City Mall, Jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Kiomoni Kibamba, amesema Baa hiyo imefungiwa, kutokana na Uongozi wa Baa hiyo kukiuka masharti ya leseni ya biashara na leseni za vileo kwa kufanya matangazo ya kibiashara kinyume na sheria ya matangazo ya vileo.
.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kwenye Baa hiyo kuna biashara mbili ya Mgahawa na Vileo ambazo zote hakuna leseni zake, kitu ambacho amesema siyo utaratibu wa kuendesha mambo, hivyo wamezuia kwa muda mpaka utaratibu ufuatwe. #via #mwananchi