Back to top

Upandaji zao la chikichi kuanza Oktoba mwaka huu.

23 May 2020
Share

Serikali imesema upandaji wa zao la michikichi utaanza rasmi Oktoba mwaka huu na kama kuna mtu mmoja mmoja au kikundi anataka kulima zao hilo aaandae shamba lake na miche ya awali atapewa bure.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema hayo baada ya kukagua kitalu cha miche ya michikichi cha Halmashauri ya Kigoma Ujiji pamoja na kitalu cha JKT Bulombora akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.

Amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, ahakikishe Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Bulombora inapewa ardhi iliyoomba kwa ajili ya kupanua kilimo cha michikichi.

Waziri Mkuu Waziri Mkuu amesema Tanzania haitaagiza mbegu za michikichi kutoka sehemu yoyote duniani, badala yake itazalisha mbegu zake na tayari ina miche milioni moja nukta nane na wataalamu wake wanaendelea kuzalisha.