Back to top

UPATIKANAJI CHAKULA SHULENI KUONGEZA AFYA YA AKILI.

16 September 2022
Share

Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, imesema kuwa , ili kupata matokeo mazuri ya elimu, ni lazima kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora shuleni, ili kuwajengea wanafunzi afya bora, na kupata utulivu wa akili wawapo madarasani.

Akizungumza jijini Dodoma, wakati wa hafla fupi ya utiaji saini fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni, Naibu Waziri wa Elimu Mh.Omary Kipanga, amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa sera hiyo, utoaji wa huduma ya chakula shuleni umekuwa ukitekelezwa katika shule kwa namna na viwango tofauti.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson amesema kuwa moja ya njia ya kufikia malengo kwa taifa lolote Duniani ni lazima kuwekeza kwa watoto hivyo ili kufikia huko lishe ni eneo linalohitaji maboresho makubwa.

Naye Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Shirika la Mpango Chakula Duniani (WFP) Dodoma  Nima  Sitta amesema ni Muungano wa kimataifa wa chakula shuleni ni jukwaa la kuhakikisha nchi zote duniani ifikapo 2030 kila mtoto anapata angalau mlo mmoja shuleni.