
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imesema mamlaka husika hazina budi kukamilisha upelelezi wa kesi za ugaidi na uhujumu uchumi ambazo inashindwa kuzisikiliza huku ikiwa inawajibika kwa wananchi.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Zainabu Muruka amesema katika ziara alioifanya hivi karibuni katika magereza kanda ya Mtwara amekumbana na changamto hizi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Danstani Kyoba amesema nilazima mawakili wabadilike ili kwenda sambamba na kasi ya utendaji kazi wa mahakama kwa sasa.
