
Meneja wa vivuko, Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kanda ya mashariki na kusini, Lukombe King'ombe amesema kuwa kukwama kwa kivuko cha MV Magogoni kinachotoa huduma zake kati ya Kigamboni na Magogoni mkoani Dar es Salaam kumesababishwa na upepo uliokisukuma mpaka ufukweni kwenye kina kifupi cha maji na kupelekea kivuko hicho kukwama.
.
Hata Hivyo, Meneja huyo amebainisha kuwa tayari Kivuko hicho kimeshanasuliwa.
