Back to top

Upungufu matundu ya vyoo, Wanafunzi 449 watumia matundu 4 ya vyoo.

22 January 2021
Share

Shule ya msingi Shikizi Kiyegea iliyopo manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro yenye wanafunzi 449, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo, madarasa pamoja na madawati ambapo hali hiyo imesababisha asilimia 75 ya wanafunzi kukaa chini.

Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Faidha Mmbaga ambapo amesema kuwa shule hiyo ina matundu manne pekee ambayo yanatumiwa na wanafunzi 449, hivyo ameomba wadau na seriakli kuisaidia shule hiyo.

Amesema kuwa shule hiyo kwa sasa ina upungufu wa madarasa pamoja na madawati jambo ambalo wanafunzi wanalazimika kukaa chini.

Kwa sasa kumekuwa na upungufu mkubwa wa madarasa na madawati katika shule mbalimbali za Msingi na za Sekondari ambazo zinamilikiwa na Serikali.