Back to top

URUSI KUSHIRIKIANA NA AFRIKA KUKUZA UCHUMI

29 July 2023
Share

Serikali ya Urusi imeahidi kushirikiana na nchi za Bara la Afrika, ikiwemo Tanzania katika kuboreha uchumi.
.
Hayo yemesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Pili wa Kilele, baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, uliofanyika katika kituo cha  mikutano cha Expo Forum, kilichopo Jijini St. Petersburg, Urusi.
.
Aidha, Waziri Mkuu amebainisha kuwa, wamesisitiza matumizi ya nishati mbadala kama njia muhimu ya kuwawezesha wananchi wa vijijini, ili nao waweze kuimudu na kuitumia katika kukuza uchumi wao.