Back to top

Ushahidi wa video ‘ajali ya ndege ya Ukraine’ Iran yanyooshewa kidole.

10 January 2020
Share

Ushahidi wa video umeonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora la Iran ndio liliiangusha kwa bahati mbaya ndege ya Ukraine iliyokuwa na abiria 176 wakati wakitekeleza shambulio dhidi ya kamba za jeshi za Marekani zilizopo Iraq.

Ndege  hiyo ilianguka dakika kadhaa baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini nchini Iran wakati kukiwa na mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran ,wote waliokuwa kwenye ndege hiyo kufariki.

Nchi za Magharibi zimetaka uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia tukio hilo.