Back to top

USULUHISHI WA MIGOGORO KATIKA JAMII WAPUNGUZA KESI

24 January 2023
Share

Utatuzi mbadala wa migogoro katika jamii umepunguza, kesi katika Mahakama ya mwanzo Msimbati iliyopo Wilaya ya Mtwara, kutoka 200 na kufikia 20.

Kauli hiyo imemtolewa na Karani wa Mahakama ya mwanzo katika Kata ya Msimbati, Wilaya ya Mtwara Vijijini, Musa Ally, katika wiki ya sheria inayoendelea hapa nchini.

Amesema Kata hiyo ina desturi ya kusuluhisha migogoro inayojitokeza katika jamiii, kupitia kwa viongozi waliopo katika jamii hatua iliyopunguza mashauri katika mahakama hiyo.

Akizungumzia wiki ya sheria, Jaji Mfawidhi, Kanda ya Mtwara, Zainab Muruke, amesema usuluhishi wa migogoro katika ngazi ya jamii utasaidia kupunguza gharama na muda unaotumika katika kuendesha mashauri.

Amesema kata ya Msimbati imeonesha kuwa vitendo usuluhishi wa migogoro katika ngazi ya jamii, licha ya kuwa na watu wasiopungua elfu tisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Msimbati, Issah Mkumba, amesema kipaji alichonacho cha kusuluhisha migogoro, amekirithi kutoka kwa wazazi wake.

Hata hivyo ameiomba serikali kuwawezesha kwa chochote, kutokana na kufanya kazi ngumu ya kusuluhisha wa migogoro na hivyo kuipunguzia serikali gharama ya kuendesha mashauri hayo.