Back to top

UTAPIAMLO WAPUNGUA MKOANI MTWARA

18 November 2022
Share

Tatizo la utapiamlo katika mkoa wa Mtwara limepungua, hasa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, ukilinganisha na mwaka 2015-2016.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, ametoa kauli hiyo wakati wa kusaini  mkataba wa usimamizi wa utekelezaji wa afua za  lishe na wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri.

Amesema mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa, udumavu uliokuwa asilimia 33.7 umepungua na kufikia asilimia 29.6, wakati ukondefu uliokuwa asilimia 3.2 umepungua na kufikia asilimia 1.6, huku uzito pungufu umepungua kutoka asilimia 15 na kufikia asilimia 12.

Hata hivyo , amesema pamoja na kupungua kwa viwango hivyo vya utapiamlo, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka virutubisho kwenye vyakula.

Kanali Abbas ameongeza kuwa ,mbali na chakula, mafuta ya kula pia yamekuwa yakiwekwa vitamini A ili kukabiliana na changamoto hizo, na kusisitiza elimu iendelee kutolewa , ili wananchi waweze kukabiliana na suala la utapiamlo na udumavu, ili malengo yalizowekwa na serikali ya kuwa na jamii yenye afya bora iweze kufikiwa.