Back to top

Utoaji mikopo elimu ya juu kuchunguzwa

31 July 2022
Share

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ametangaza Tume ya watu watatu itakayochunguza uhalali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 mpaka 2021/2022 ili kubaini kama kulikuwa na upendeleo kwa watu wasiokuwa na sifa.
.
Tume hiyo itaongozwa na Prof.Allan Mushi ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Idd Makame kutoka Zanzibar na Dkt.Martin Chegeni ambao wote kwa pamoja ni wataalamu wa mifumo waliobobea katika sayansi ya kompyuta na takwimu.