Back to top

UTURUKI KUPINGA MATAIFA YANAYOTAKA KUJIUNGA NA NATO

19 May 2022
Share

Rais wa Uturuki Receip Erdogan ametishia kwamba Uturuki inaweza kupinga maombi ya mataifa ya Sweden na Finland kujiunga na NATO.

Rais Erdogan amesema kwamba anatarajia washirika wa Nato kuelewa hisia za Uturuki kuhusu usalama.

Katika hotuba yake kwa wabunge wa chama chake tawala, pia alirudia maoni yake kwamba wajumbe wa Uswidi na Finland wasijisumbue kuja Uturuki kujadili masuala hayo.

Uturuki inayashutumu mataifa hayo mawili ya Nordic kwa kuwapa hifadhi wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK), kikundi ambacho inakiona kama chama cha kigaidi, na wafuasi wa Fethullah Gulen, ambaye  Uturuki a inamtuhumu kuandaa jaribio la mapinduzi ya 2016.

Kulingana na shirika rasmi la habari la Uturuki, Finland na Uswisi zimekataa maombi kadhaa ya kuwarejesha wanamgambo wa Kikurdi ambao Uturuki inawataja kuwa magaidi.