Back to top

Uturuki kusalia Libya mpaka haki ipatikane.

22 January 2020
Share

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema nchi yake itaendelea kubaki Libya mpaka pale itakapopata haki zake katika bahari ya Mediteranea,kupatikana kwa utawala halali wa Libya ikiwemo usalama na utulivu.

Rais Erdoğan, amezungumza hayo jijini Istanbul akishiriki  hafla ya kuzungumzia vyanzo vya kwanza vya mradi wa Usafiri wa Metro kuelekea uwanja wa ndege wa Istanbul.

Akizungumzia makubaliano na serikali halali ya Libya amesema makubaliano  juu ya Mediteranea yameishtua dunia nzima.