
Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uturuki (TFF), umesimamisha mechi zote katika ligi zote, nchini humo, kwa muda usiojulikana, baada ya Rais wa klabu ya MKE Ankaragucu, Faruk Koca, kumpiga ngumi muamuzi, aliyejulikana kwa jina la Halil Umut Meler, aliyekuwa akichezesha mchezo wa Super Lig kati ya timu ya MKE Ankaragucu na Caykur Rizespor ambazo zilitoka sare ya 1-1.
.
Imedaiwa kuwa Faruk Koca alikimbilia uwanjani kisha kumpiga muamuzi huyo baada ya timu yake kufungwa bao la kusawazisha dakika ya 97, huku Uongozi wa Shirikisho hilo ukisema kuwa shambulizi hilo ni aibu kwa soka la Uturuki.
.
Ikumbukwe kuwa Meler, ni mmoja wa waamuzi bora nchini Uturuki na muamuzi katika michezo ya kimataifa ya FIFA, pia yupo katika orodha ya waamuzi wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.
