Back to top

Rais Magufuli aridhia Uwanja wa Taifa uitwe uwanja wa Mkapa.

28 July 2020
Share

Rais Magufuli amesema amekubalina na maombi ya kuuita uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam, Uwanja wa Mkapa kwa kumbukumbu ya kiongozi huyo.

Katika rambirambi zao, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini waliowakilishwa na Balozi wa Comoro, wamemuelezea Hayati Benjamin Mkapa kuwa alikuwa Mwanadiplomasia makini na kuondoka kwake, Afrika na dunia imempoteza kiongozi wakati ilikuwa akihitajika.

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Lupaso, wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe AMEN.