Back to top

VAR KUTUMIKA MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA

16 December 2023
Share

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limewapa vifaa vya usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR), ambavyo vitatumika katika Ligi Kuu Tanzania Bara. 
.
Karia ameyasema hayo, leo Disemba 16, 2023, katika mkutano mkuu wa TFF, unaofanyika  mkoani Iringa, ambapo amebainisha kuwa vifaa hivyo vitafungwa katika viwanja vinavyokidhi vigezo vya CAF na shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) na kwamba tayari wataalamu wa vifaa hivyo wamefika kwa ajili ya kutoa mafunzo.
.

"Niwape habari njema kuwa tumepata VAR kutoka CAF na hii ni muendelezo wa uhusiano mzuri na CAF. Wataalam wameingia jana kutoa mafunzo. Itafungwa katika viwanja vyenye 'standard' (ubora)" Karia.