Back to top

Corona yaendelea kutafuna maisha ya watu, vifo vyafikia 1,115.

12 February 2020
Share


Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 1,115 na walioambukizwa ikifikia 45,171 huku waliopona wakifikia 4,831, Shirika la Afya Duniani limeupa jina rasmi ugonjwa huo kwa kuuita COVID-19. 

Kufuatia virusi hivyo Serikali ya China imepanga kuyaruhusu makampuni kwenye maeneo mengi isipokuwa Jimbo la Hubei, kuanza tena shughuli zao kwa sharti la kuchukua hatua stahiki kuepusha maambukizo.

Hata hivyo Februari 11, 2020 Timu ya wataalamu wa Shirika la Afya duniani ilielekea Beijing nchini China kuchunguza mlipuko wa virusi vya Corona.

Katika hatua nyingine Shirika la Afya Duniani WHO, lilisema jina rasmi la ugonjwa unaosababisha na virusi vipya vya corona uitwe Covid-2019.

"Sasa tumeupatia jina ugonjwa na utaitwa Covid-19," Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

Watafiti wamekua wakitoa wito wa kuwepo kwa jina rasmi ili kuepuka mkanganyiko na unyanyapaa.