
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kwa 50% kutoka vifo 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020 huku maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima yakishuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020 na maambukizi mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto yakishuka kutoka 18% mwaka 2010 hadi 7% mwaka 2020.
.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo kwenye harambee ya uchangishaji wa fedha za kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka 2022.
.
Aidha, Mhe.Simbachawene amebainisha kuwa tayari serikali imetenga fedha Bilioni 1.88 kwenye bajeti ya 2022/2023 ili iendelee kuchangia AIDS TRUST FUND.
