Back to top

VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI VYAONGEZEKA MAREKANI

05 July 2023
Share

Vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi nchini Marekani, vimeongezeka zaidi ya mara mbili katika miongo miwili iliyopita, huku wengi wanaokumbwa ni wanawake wenye asili ya Afrika.

Utafiti uliochapishwa katika Jarida la Jumuiya ya Madaktari ya Marekani, umeonesha kuwa wanawake wengi wenye asili ya Afrika, India na Alaska, wamefariki dunia katika taifa hilo, kutokana na matatizo ya uzazi.

Mmoja wa watafiti Dakta Allison Bryant, amesema ripoti hiyo inaonyesha kuwepo ubaguzi wa rangi katika sekta ya tiba.