Back to top

VIFO WALIOKULA NYAMA ROMBO, SIO KIMETA

25 May 2023
Share

Wizara ya Uvuvi na Mifugo imesema vifo vya watu wawili vilivyotokea baada ya kula nyama kwenye Kijiji cha Msaranga kilichopo Kata ya Kisale, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro Mei 4, 2023, havihusiani na ugonjwa wa kimeta.
.
Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mifugo Tanzania Dkt. Benezeth Lutege, Wizara hiyo imewasisitiza wananchi waote kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya ikiwemo kununua nyama zilizokaguliwa na wataalamu wa mifugo waliosajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) na kutoka kwenye mabucha yaliyothibitishwa na Bodi ya Nyama nchini.