Back to top

VIJANA 32 WAPEWA VITAMBULISHO VYA VGS.

15 December 2023
Share

Vijana 32 wa vijiji vya Mlazo na Ndogowe kata ya Nghambaku Wilayani Chamwino Mkoani Dododma wamekabidhiwa vitambulisho vya kuwatambua rasmi kuwa ni Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) baada ya kuhitimu mafunzo  katika Chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori Likuyu Sekamaganga kilichopo Mkoani Ruvuma. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Katibu Tawala wa Wilaya ya Chamwino Bi Neema Nyalege amesema vitambulisho hivyo vitawapa askari hao nguvu za kisheria za kutekeleza majukumu ya uhifadhi.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Kay Kagaruki amesema Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara kwa ufadhili wa mfuko wa Mazingira Duniani iliwezesha ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhi kwa kuanza mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Chamwino.